Hungary yatishia kuzuia vikwazo vipya vya EU dhidi ya Urusi
13 Mei 2023Ni baada ya benki kubwa ya biashara nchini Hungary, OTP kuorodheshwa kuwa miongoni mwa taasisi ambazo huenda zitalengwa na vikwazo hivyo.
Mwanadiplomasia huyo amesema iwapo benki hiyo itaendelea kuwemo kwenye orodha iliyotolewa na Ukraine ya taasisi zinazoiunga mkono Urusi, nchi yake haitaidhinisha duru mpya ya vikwazo.
Soma zaidi:Hungary yalegezewa masharti na EU iunge mkono vikwazo vya mafuta dhidi ya Urusi
Akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Umoja wa Ulaya unaofanyika nchini Sweden, Szijjártó, amesema ni jambo la kashfa kwa Ukraine kuijumuisha benki hiyo katika orodha yake wakati haijakiuka sheria yoyote.
Ukraine inaizingatia benki ya OTP kuwa taasisi yenye ushirika wa karibu na Urusi na inaituhumu kufadhili shughuli za kifedha za Moscow.