Hungary huenda ikaondoa pingamizi lake la msaada kwa Ukraine
17 Januari 2024Matangazo
Von der Leyen ameliambia bunge la Ulaya kwamba ana imani kuwa suluhu juu ya mkwamo huo itapatikana.
Mnamo mwezi Disemba, mwaka jana Waziri Mkuu wa Hungary mwenye kuegemea siasa za mrengo wa kulia Viktor Orban, ambaye pia ni mshirika wa karibu wa Urusi, alikataa kutia saini msaada zaidi wa kifedha kwenda kwa Ukraine.
Blinken asema Marekani itaendelea kuisaidia Ukraine
Viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya walikubaliana kufanya tena mkutano mjini Brussels Februari 1 ili kujaribu kuishawishi Budapest kubadili msimamo wake, pamoja na kujadili kwa upana juu ya bajeti ya umoja huo.