1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Human Rights Watch yaitaka Kenya kuwajibika

Kalyango Siraj16 Oktoba 2008

Watu 1,100 walifariki katika ghasia za uchaguzi Kenya

https://p.dw.com/p/FbS9
Moja wa tukio la ghasia za kikabila Kenya baada ya uchaguzi wa 2007Picha: Picture-Alliance /dpa

Shirika la kimataifa linaloteta haki za binadamu la Human Rights Watch limeitaka serikali ya Kenya kuheshimu mapendekezo ya tume ya Hakimu Phillip Waki iliochunguza ghasia zilizofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Miongoni mwa mengine tume hiyo,iliochapishwa jumatano, ilipendekeza kuundwa kwa mahakama maalum itakayowashughulikia waliochochea na kuhusika katika ghasia hizo zilizopekea watu kadhaa kuuawa na wengine kuachwa bila makazi.

Mwito huo umo katika taarifa ya shirika hilo iliotolewa alhamisi.Shirika hilo limetaka sio tu serikali ya Kenya,lakini pia washirika wa kimataifa, kuunga mkono mwito wa tume ya Waki wa kuundwa kwa mahakama maalum kwa lengo la kukomesha hali ya watu kutowajibika na makosa wanayotenda unaondelea nchini Kenya.

Mkurugenzi wa meza ya Afrika ya shirika la Human Rights Watch, Georgette Gegnon,amesema kuwa tume ya Waki ilifanya kazi kubwa nzuri ambayo imeeleza chanzo cha ghasia hizo pamoja na kuchukua ushaidi.Afisa huyo ameongeza kuwa kutokana na kuwa haki ni muhimu kwa ajili ya amani ya Kenya,wanasiasa sasa wanawajibika kuunda mahakama maalum iliopendekezwa.

Ripoti ya tume ya Waki, miongoni mwa mengine, ilisema kuwa wanasiasa wa pande zote walihusika, kwa njia moja ama nyingine, katika kuandaa na kufadhili mashambulizi dhidi ya wafuasi wa upinzani.Hassan Omar Hassan , makamu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya Kenya haki za binadamu anasema kuwa hatua iliochukuliwa ilikuwa sawa.

Aidha ripoti hiyo inavilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wa kawaida. Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa serikali imechelewa kufanya mabadiliko katika jeshi la Polisi kama ilivyopendekeza tume ya wako.

Kuhusu kuundwa kwa mahakama maalum kuwashughulikia wahusika, tume imependekeza kuwa endapo mahakama hiyo haitaundwa au juhudi zake kuzuiliwa basi majina ya wahusika ambayo imeyahifadhi yapewe mahakama ya kimataifa ya makosa jinai ya mjini The Hague Uholanzi.

Afisa wa shirika la Human Rights Watch amesema kuwa uongozi wa Kenya unapashwa kuachana na yaliyopita na kushunghulikia mapendekezo ya tume ya Waki kama ilivyo la sivyo,imesema ni wakenya wenywewe ndio wataumia kutoan na ghasia zingine za hapo usoni.

Takriban watu 1,100 waliuawa na wengine 300,000 kuachwa bila makazi kutokan na ghasia baada ya uchaguzi mkuu wa Disemba 2007.Na tume ya Waki imechapisha jumatano matokeo ya uchunguzi wake ulidumu miezi mitatu.