1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Human Rights Watch laomba polisi ya Kenya kutotumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cp3C

NAIROBI:

Shirika linalotetea haki za binadamu la Marekani-la Human Rights Watch limeiomba serikali ya Kenya kuamuru askari wake polisi wanaotuliza ghasia kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.Katika taarifa ya shirika hilo iliotolewa jumapili mjini Nairobi na kaimu mkurugenzi wa tawi la Afrika la shirika hilo-Georgette Gagnon, shirika la Human rights Watch limetoa mwito kwa serikali kukubali wananchi kutoa maoni yao. Mwito huo umekuja wakati wafuasi wa Bw Odinga wakipanga maandamano wiki ijayo. Serikali imepiga marufuku maandamano yote tangu kutangazwa kwa matokeo ya urais yaliyomrejesha madarakani rais Mwai Kibaki.Matokeo yanapingwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga akidai kulifanyika mizengwe na kusema maandamano yataendelea.Lakini msemaji wa serikali ya Kenya Alfred Mutua amelaani hatua ya kuitisha maandamano hayo.

‚Amesema kuwa ni lazima wananchi waepuke na miito ya kufanya ghasia pamoja na maandamano ambayo hayaleti tija kwa maisha ya mwanadamu, bali kuondeleza chuki za kisiasa za watu wachache. Aongeza kuwa tofauti ya kisiasa zisipelekwe barabarani.Na badala yake zitumiwe njia zilizopo na kuiheshimu katiba ya taifa na pia kuheshimiana.’

Ghasia za kikabila na kisiasa zilizofuata kutangazwa kwa matokeo hayo zimesababisha idadi ya waliopoteza maisha yao kufikia 700 ushei kwa sasa .Hii ni kwa mujibu wa polisi.