Hukumu ya gaidi mtuhumiwa Munir Mutassadeq itatangazwa jumatatu ijayo mjini Hamburg
6 Januari 2007Matangazo
Hambourg:
Hukumu dhidi ya Mounir El Motassadeq anaetuhumiwa kuwasaidia magaidi walioshirikiana na Mohammed Attah mjini Hambourg,inatazamiwa kutolewa jumatatu ijayo.Itatangazwa mapema zaidi kuliko ilivyokua imepangwa hapo awali.Raia huyo wa Moroko anaendelea kudai hana hatia.Anatuhumiwa kusaidia maandalizi ya mashambulio ya september 11 mwaka 2001 nchini Marekani.Katika awamu hii ya tatu ya kusikiliza kesi dhidi yake,mahakama ya mjini Hambourg inahitaji kutangaza hukumu tuu itakua ya muda gani.Wadadisi wanaamini Munir Mutassadeq huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.