1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Huenda Pogba akafungiwa kandanda kwa miaka minne

7 Desemba 2023

Mchezaji wa kandanda wa timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba anakabiliwa na uwezekano wa kufungiwa kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4ZtJl
Frankreich | Mathias Pogba im Elysee-Palast in Paris
Paul Pogba akiwa Elysee-Palast huko ParisPicha: Moritz Thibaud/ABACA/picture alliance

Mchezaji ni baada ya mahakama ya kitaifa ya Italia inayopambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini kutaka kiungo huyo wa Juventus afungiwe kwa miaka minne.

Soma pia: Dawa za kusisimua misuli: Paul Pogba asimamishwa kwa muda

Pogba, 30, alipigwa marufuku kucheza kandanda mwezi Septemba baada ya kukutwa na dawa ya kututumua misuli, mwezi mmoja baadaye sampuli B ilithibitisha kuwepo kwa dawa hizo.

Kesi yake inaendelea katika Mahakama ya michezo nchini huku ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Turin pia imeanzisha uchunguzi wa mahakama, kwani dawa za kuongeza nguvu ni kosa la jinai nchini Italia.

"Ninaweza kuthibitisha kwamba tulipata taarifa hii asubuhi kutoka kwa wakala wa kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli iliyoomba kupigwa marufuku kwa miaka minne," chanzo cha Juve kiliiambia AFP.

Sampuli za mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2018 akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa ziliripotiwa kuchukuliwa katika mechi ya ufunguzi ya klabu yake ya Juventus kwenye ligi ya Serie A, ambapo walipata ushindi dhidi ya Udinese mnamo Agosti 20, ambapo alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumiwa. 

Paul Pogba | französischer Fußballspieler
Paul Pogba akiwa uwanjani wakati akiichezea JuventusPicha: Claudio Benedetto/ZUMAPRESS/picture alliance

Wawakilishi wa Pogba walisema testosterone hiyo ilitokana na kirutubisho cha chakula kilichowekwa na daktari ambaye alishauriana naye nchini Marekani.

Chini ya Kanuni ya Kuzuia Matumizi ya Madawa ya Kulevya Duniani, Pogba anawajibika kufungiwa kwa miaka minne, ambayo inaweza kupunguzwa kwa nusu ikiwa atathibitisha kwamba hakuwa na makosa.

Marufuku hiyo inaweza hata kupunguzwa kwa miezi michache ikiwa matumizi  yalifanyika "nje ya ushindani na haihusiani na kiwango chake cha utendaji uwanjani".

Tangu kutangazwa kwa vipimo vyake, Pogba ameshindwa kufanya mazoezi na Juventus, ambapo alitua mnamo Julai 2022 baada ya misimu sita na Manchester United.  Juve pia wamesitisha malipo ya wastani wa mshahara wake wa kila mwaka wa euro milioni 8.