Wabunge wa Kenya wamepitisha muswada utakaowawezesha kutia kibindoni kitita cha shilingi 100,000 za kenya sawa na dola 1000 kila mwezi kama pensheni baada ya kustaafu. Muswada huo unaosubiriwa kutiwa saini na rais kuwa sheria, utawanufaisha wabunge waliohudumu kati ya mwaka 1984 na 2001. Zaidi sikiliza mahojiano haya kati ya Tatu Karema na Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Kenya Herman Manyora.