Huduma za kiutu zaruhusiwa upya Somalia
5 Desemba 2007Matangazo
Nchini Somalia,huduma za misaada ya kiutu zimeanzishwa upya leo hii baada ya serikali kuzuia huduma hizo,siku ya Jumanne kwa sababu zisizojulikana.Hatua ya kuzuia misaada hiyo ya kiutu ilichukuliwa siku moja baada ya afisa wa misaada wa ngazi ya juu,John Holmes kuizuru Somalia.Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa aliahidi kugombea uhuru zaidi kwa harakati za kiutu.
Tangazo la siku ya Jumanne,lilihatarisha operesheni za WFP-Shirika la Mipango ya Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa.Chakula hicho kinapelekwa kwa maelfu ya watu waliokimbia mapigano katika mji mkuu Mogadishu na sasa huishi kambini ukingoni mwa mji huo.