Homa ya manjano husababisha vifo vya watoto karibu 30,000 kila mwako kote ulimwenguni, huku asilimia 90 wakiwa ni kutoka mataifa ya Afrika. Ili kukabiliana na hali hiyo, shirika la kimataifa la WHO limeendesha kampeni kabambe inayolenga kuusambaratisha ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030, suala linaloangaziwa hii leo kwenye makala ya Afya yako iliyoandaliwa na Lubega Emmanuel.