1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hollande aahidi usalama katika Euro 2016

6 Juni 2016

Ufaransa imeahidi kuchukua kila hatua ili kuhakikisha usalama wa wote watakaoshiriki katika mashindano hayo. Rais Francois Hollande amekiri kuwa kuna kitisho cha mara kwa mara ambacho lazima kishughulikiwe

https://p.dw.com/p/1J1Ol
Frankreich Terroranschläge Polizei
Picha: picture-alliance/dpa/G. Horcajuelo

Hollande amesema anatumai dimba hilo litawaleta pamoja watu wa Ulaya wakati kukiwa na mizozo ya kisiasa ukiwemo mgogoro mkubwa kabisa wa wakimbizi kuwahi kushuhudiwa barani humo "Kitisho cha kinyang'anyiro sio namna kitakavyokwenda. Wajibu wangu ni kufanya Euro 2016 iwe sio tu tamasha la kuvutia la michezo, lakini pia kitu kinachowaleta pamoja watu wa Ufaransa, Ulaya, na watu ambao hawangekuwa na fursa ya kukutana. Na hilo kawaida ndio jukumu la michezo".

Ufaransa ilirefusha amri ya hali ya hatari, iliyowekwa baada ya mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, hadi Julai 26 ili kujumuisha mashindano maarufu ya baiskeli ya Tour de France Julai 2-24.

Pia amekanusha madai yaliyotolewa na nyota wa Real Madrid Karim Benzema, aliyesema kuwa alinyimwa nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa kwa sababu ya mizizi yake ya Kialgeria. "Kuna kocha mmoja tu – Didier Deschamps. Anawachagua wachezaji anaohisi wanapaswa kuwa katika timu ya Ufaransa katika mazingira ya sasa ya kinyang'anyiro hiki. Inasikitisha kwa wale ambao hawakufaulu kujumuishwa kikosini lakini ndio kigezo pekee kilicho na maana, Uamuzi wa kocha".

Michuano ya Euro 2016 inang'oa nanga katika Stade de France mnamo Juni 10 na itamalizika Julai 10

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri:Iddi Ssessanga