Dilma Rousseff,hii leo anasubiri uamuzi wa baraza la Senete
30 Agosti 2016Rais Rouseff anatuhumiwa kuivunja sheria ya bajeti mwaka 2014,ili kuficha hali mbaya ya kiuchumi inayokabili taifa hilo,tuhuma alizokanusha vikali. Baraza la Senete linatazamiwa leo kusikiliza hoja za mwisho kutoka kwa mawakili wa pande zote mbili, kabla ya kikao cha mwisho ili kufanyika kura hiyo ya kuamua hatma ya rais Rouseff. Kikao hicho kinatazamiwa kuendelea hadi kesho. Ili kumuondoa madarakani rais Rouseff Thuluthi mbili au maseneta 51 miongoni mwa 81 wanapaswa kupiga kura kuunga mkono wazo hilo.
Hata hivyo Rouseff ambae ni rais wa kwanza mwanamke nchini Brazil ameshikilia kuwa tuhumu zinazomwandamana hivi sasa zimepangwa na na wale ambao aliwashinda katika uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita. Akikumbuka mateso aliyoyapitia kuizuizini wakati wa utawala wa kiimla wa kijeshi nchini humo miaka ya 70 ,kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto aliwataka maseneta kupinga kura hiyo ya kumtimua." Huu ni mchakato ulioanza pengine baada ya kukamilika muhula wangu wa kwanza ,lakini ukashika kasi katika muhula wangu wa pili wa uongozi.Wakati muungano wa democrasia na maendeleo inaungana na kuwa muungano wa mapinduzi " alisema Rouseff.
Huenda nafasi ya rais Rouseff ikachukuliwa na makamu wake Michel Temer ambae amebadilika na kuwa hasimu wake mkubwa.Temer alisema anautazama mchakato mzima kwa utulivu.Iwapo baraza la seneti litaridhia kumg'oa madarakani rais huyo Temer ataapishwa kuwa rais wa Brazil mpaka mwaka 2018 kutakapofanyika uchaguzi mkuu.
Licha ya hayo kumekuwa na maandamano yanayomuunga mkono Rousseff katika maeneo mbalimbali nchini humo wengi wao kutoka chama chake cha workers party. Chama hicho chini ya Rouseff na mtangulizi wake Luiz Lula da Silva kinasifa ya kuwaondoa karibu wabrazil million 29 katika lindi la umaskini.
Hata hiyo Wabrazil wamewageukia viongozi wao na kuwalaumu kutokana na maovu yanayoendelea nchini humo huku wakismhtumu Rouseff kwa uendeshaji mbaya wa nchi. Kuondolewa kwa rais huyo mamlakani kutatamatisha uongozi wa miaka 13 wa chama cha mrengo wa kushoto cha Workers Party. Utawala wake umegubikwa na kashfa kadhaa za ufisadi na kusababisha mzozo mbaya zaidi ya kisiasa. Uchumi wa Brazil ulishuka hadi asilima 3.8 mwaka 2015 na kuna uwezekano ukashuka zaidi kwa asilima 3.3 mwaka huu hii ikiwa hali mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 1930.
Mwandishi: Jane Nyingi/AFPE/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga