Hofu yatanda juu ya kusambaa kwa UVIKO-19
29 Desemba 2022Marekani inachukua hatua hiyo wakati visa vya maambukizi ya UVIKO-19 vikiongezeka nchini China. Hospitali kote China zimelemewa na mripuko wa maambukizi kufuatia uamuzi wa Beijing kuondoa kanuni kali ambazo kwa kiasi kikubwa zilikuwa zimekidhibiti kirusi hicho lakini zikaathiri uchumi na kuzusha maandamano makubwa. Marekani na nchi nyingine kadhaa zimetangaza kuwa zitahitaji matokeo ya vipimo vya UVIKO kutoka kwa wasafiri wote wanaotokea China bara. Hatua ya Marekani inajiri baada ya Italia, Japan, India na Malaysia kutangaza hatua zao katika jitihada za kuepusha kuingiza katika nchi zao aina mpya ya virusi kutoka China. Halmashauri Kuu ya Ulaya inakutana leo kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO nchini China.