Hivi karibuni, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonyesha utayari wa kutuma wanajeshi wa nchi yake nchini Ukraine iwapo serikali ya Volodymr Zelenskiy itaomba msaada huo. Kauli yake imezua wasiwasi juu ya kutanuka kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine. Babu Abdalla amezungumza na mchambuzi wa siasa za kimataifa na mwandishi mstaafu wa DW Kiswahili Abdul Mtullya kuhusu wasiwasi huo.