1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu hospitali za Gaza wakati mafuta na misaada vinapungua

23 Novemba 2024

Wizara ya afya ya Gaza imesema hospitali zimesalia na siku mbili tu za mafuta kabla ya kuzuia huduma, baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kwamba utoaji wa misaada katika eneo lililoharibiwa na vita umetatizwa.

https://p.dw.com/p/4nLjU
Gaza Grenzübergang Rafah
Mtoa tiba akimuhamisha mtoto mchanga njiti kutoka Ukanda wa Gaza katika eneo la kivuko cha Rafah Novemba 20, 2023.Picha: Egypt's State Information Center/Xinhua/picture alliance

Onyo hilo la wizara hiyo inayodhibitiwa na kundi la Hamasliimekuja siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kutoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa ulinzi Yoav Gallant ikiwa ni zaidi ya mwaka tangu kuanza kwa vita vya Gaza. Madaktari wa Gaza wamesema uvamizi wa Israel wa usiku wa kuamkia leo katika miji ya Beit Lahia na karibu na Jabalia ulisababisha idadi kadhaa ya watu kuuawa au kutoweka. Mara kwa mara Umoja wa Mataifa na mashiriki mengine ya misaada ya kiutu umeelezea hali ya kibinadamu, haswa kaskazini mwa Gaza, ambapo Israeli ilisema Ijumaa iliwaua makamanda wawili waliohusika katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 ambalo ndio kiini cha vita.