Hisia kutoka Zanzibar kuhusu kifo cha Benjamin Mkapa
24 Julai 2020Anakumbukwa kwa kuleta mabadiliko katika mfumo wa sera za fedha Tanzania na kufufua viwanda.
Lakini kwa upande hasi atakumbukwa sana kwa tukio maarufu ya mauaji ya Januari 26 na 27 2001ambapo zaidi ya watu 30 waliuawa na wengine 4,000 kuikimbia nchi.
Ingawa yeye mwenyewe Rais Mkapa aliyeeleza tukio hilo lilitia doa katika utawala wake ndani ya kitabu alichoandika kiitwacho My life My Purpose, wapo wanaosema hakuomba radhi kama ilivyopaswa kwa roho zilizopotea.
Pamoja na tume iliyoundwa kufanya uchunguzi wa tukio hilo ya Jenerali Hashim Mbita kutomtia hatiani au kuweka lawama kwa mtu yeyote Yule au walau kulipwa fidia waathirika ndio inaongeza kumbukumbu kwa wazanzibari kutoyasahau matukio hayo machungu.
Suala hilo la mauaji yalichangia kupatikana kwa Muafaka kati ya vyama viwili vya CCM na CUF.
Miongoni mwa mambo ambayo Mzee Mkapa katika kipindi chake alijitahidi sana kuwataka Wazanzibari kulinda ni Mapinduzi na kuutetea Muungano kwa nguvu zote.
Mwandishi: Salma Said DW Zanzibar