1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton nchini Israel

3 Machi 2009

Kabla mkutano na Netanyahu

https://p.dw.com/p/H4oP
Hillary Rodham Clinton, Shimon Peres .Picha: AP

Waziri wa nje wa Marekani bibi Hillary Clinton, anatazamiwa hivi punde kukutana na Benjamin Netanyahu Kiongozi wa chama cha LIKUD baada ya mazungumzo yake hapo kabla leo na waziri wa nje na Kiongozi wa chama cha KADIMA Bibi Tzipi Livni.

Katika mkutano na waandishi habari pamoja na Bibi Livni, Bibi Clinton aliahidi kusukuma mbele huhudi za kuundwa kwa dola huru la wapalestina-hatua ambayo itaugonganisha uso kwa uso utawala wa rais Obama mjini Washington na ule wa wsaziri-mkuu-mteule Benjamin Netanyahu asiewafiki tangu kugawanywa kwa mji mkuu wa jeruselem hata na kuundwa kwa dola la wsapalestina.

"Ni makisio yetu kuwa mwishoe haitaepukika kuwa na suluhisho la dola 2." alisema bibi Clinton.

Waziri-mkuu-mteule Benjamin Netanyahu anazungumzia tu kuwaachia wapalestina kujitawala wenyewe lakini hadi sasa anakwepa kuzungumza wazi kuwa anaungamkono mfumo wa dola mbili-ile ya Israel na ya wapalestina kama njia ya ufumbuzi wa mgogoro wa mashariki ya kati.

Bibi clinton alisema:"Tutashirikiana kupeleka mbele dhamana tulitoa kwa utawala wa rais Mahmud Abbas na waziri mkuu Fayad na kusaidia kuinyosha njia ya kuundwa dola huru la na imara wapalestina ,litakalo wajibika na kuishi kwa amani."

Akifanya leo mazungumzo mjini jeruselem baada ya kuhudhuria jana mkutanow awafadhili juu ya kuijenga upya Gaza ,huko Sharm el Sheikh, nchini Misri, waziri wa nje wa Marekani alisisitiza tena mawazo ya utawala wa Rais Barack Obama ya kufikia amani baina ya waisraeli na wapalestina.

Lakini wachunguzi wanaona kuungamkono kwa Benjamin Netanyahu hatua za kupanua zaidi maskani za walowezi wa kiyahudi katika Ukingo wa magharibi unaokaliwa n a Israel-siasa ambayo haikubaliwi na Marekani na kutoafiki kuwapo kwa dola m,bili ile ya Israel na ya wapalestina ni swali nyeti katika usuhuba kati ya Israel na Marekani.

Hatahivyo, Bibi Hillary Clinton asema Marekani itashirikiana na serikali iliochaguliwa kidemokrasi na waisraeli:

"Nataka mjuwe kwamba tutashirikiana na serikali ya Israel inayowakilisha chaguo la kidemokrasi la watu wa Israel."

Hamas inayodhibiti mwambao wa gaza na iliochaguliwa kidemokrasi ,haiwezi kutazamia ushirikiano kama huo kutoka Marekani.

Akizungumza na maripota hapo kabla baada ya kukutana na rais Shimon Perez wa Israel, Bibi Hillary Clinton aliahidi mshikamano usiorerega wa Marekani kwa Israel.

Halkadhalika, Bibi Clinton alikariri nia ya Marekani ya kuizuwia Iran isimiliki silaha za nuklia,lakini alikataa kugusia chochote kuhusu taarifa kwamba Marekani imejitolea kwa Urusi kuridhiana nayo juu ya kuachana na mradi wake wa makombora huko ulaya ya Mashariki iwapo Urusi,itaizuwia Iran na mradi wake wa kinuklia.

Bibi Clinton anatazamiwa hivi punde kuonanana na kiongozi wa Likud ,Benjamin Netanyahu kusikiliza mlio.