1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hillary Clinton amuidhinisha Barack Obama

P.Martin8 Juni 2008

Hillary Clinton alietaka kuwa rais wa kwanza wa kike nchini Marekani,amefunga kampeni zake kugombea wadhifa huo.

https://p.dw.com/p/EFdw
Sen. Hillary Rodham Clinton, D-N.Y., pauses before addressing supporters at the National Building Museum in Washington, Saturday, June 7, 2008, as she suspends her campaign for president. (AP Photo/Ron Edmonds)
Seneta Hillary Rodham Clinton,kabla ya kuwahotubia wafuasi wake mjini Washington Juni 7, 2008.Picha: AP

Clinton amesema,anamuunga mkono Barack Obama kama mgombea mteule wa chama cha Demokratik kuwania kiti cha urais nchini Marekani.Alipohotubia umati wa kama watu 2,000 Clinton aliwahimiza wafuasi wake kumuunga mkono Barack Obama na akaongezea:

"Njia ya kuendelea kugombea na kutimiza malengo yao ni kumuunga mkono Barack Obama kwa kila njia ili apate kuchaguliwa rais mpya wa Marekani. "

Barack Obama akamshukuru mpinzani wake wa zamani Hillary Clinton.Amsema ana hakika kuwa Clinton atakuwa na jukumu muhimu katika kampeni ya uchaguzi ujao. Amesema,Clinton atakuwa mstari wa mbele kugombea kuleta mageuzi nchini Marekani.

Barack Obama mwenye miaka 46 anatazamiwa kupambana na John McCain wa chama cha Republikan tarehe 4 Novemba.