1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hezbollah yatangaza "ushindi" dhidi ya Israel

28 Novemba 2024

Kundi la Hezbollah limedai "ushindi" dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo.

https://p.dw.com/p/4nVRt
Lebanon Beirut | Wakazi wa kusini mwa Beirut wakirejea nyumbani
Raia wa Lebanon waliohama makaazi yao wakirejea baada ya makubaliano ya kusitisha vita.Picha: ANWAR AMRO/AFP/Getty Images

Kundi la Hezbollah limedai "ushindi" dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo.

Licha ya vikosi vya Israel kusababisha hasara kubwa kwa kundi hilo, ikiwwemo kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, limesema Israel ilishindwa kukalia miji yoyte au kuunda eneo la usalama.

Soma pia: Viongozi mbalimbali wapongeza makubaliano ya usitishwaji vita Lebanon

Mkataba wa kusitisha mapigano unaitaka Hezbollah kuondoka kaskazini mwa Mto Litani na kuvunja miundombinu yake ya kijeshi kusini mwa Lebanon.

Hezbollah pia ilidai kufanya zaidi ya operesheni 4,637 za kijeshi dhidi ya Israel tangu Oktoba 2023 na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina.