1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Hezbollah: Israel haiwezi kuweka masharti ya kusitisha vita

21 Novemba 2024

Kiongozi wa kundi la Hezbollah Naim Qassem, amesema Israel haiwezi kuweka masharti ya kusitisha mapigano nchini Lebanon, huku mjumbe wa Marekani Amos Hochstein akielekea Israel kujaribu kusuluhisha vita hivyo.

https://p.dw.com/p/4nElt
Kiongozi wa kundi la Hezbollah Naim Qassem
Kiongozi wa kundi la Hezbollah Naim QassemPicha: Houssam Shbaro/Anadolu/picture alliance

Kiongozi wa kundi la Hezbollah Naim Qassem, amesema Israel haiwezi kuweka masharti ya kusitisha mapigano nchini Lebanon, huku mjumbe wa Marekani Amos Hochstein akielekea Israel kujaribu kusuluhisha vita hivyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Gideon Saar, alisema makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano lazima yahakikishe Israel inaendelea kuwa na "uhuru wa kuchukua hatua" dhidi ya Hezbollah.

Soma: Mjumbe: makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hezbollah

Hochstein, akiwa Beirut, alisema vita vilivyoshika kasi tangu mwishoni mwa Septemba vinaweza kufikia mwisho, huku akisisitiza haja ya kusitisha mashambulizi ili kulinda mamlaka ya Lebanon na kuwasaidia wakimbizi kurejea makwao. Vita vya Israel vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, huku Lebanon na Syria pia zikiathiriwa na mashambulizi ya Israel dhidi ya ngome za Hezbollah.