Hezbollah yaapa kulenga maeneo mapya ya Israel
17 Julai 2024Kundi hilo limekuwa likipambana na mashambulizi ya kila siku na vikosi vya Israel katika kile wanachodai ni kuunga mkono washirika wao wa Hamas.
Haya yanajiri baada ya shirika la Habari la serikali ya Lebanon kuripoti kuwa mashambulizi ya Israel kusini mwa nchi hiyo yameua watu watano wakiwemo watoto watatu wa Syria siku ya Jumanne.
Nasrallah ameionya Israel juu ya matokeo ya uvamizi wowote nchini Lebanon, akisema Israel itaachwa bila mizinga yoyote iwapo mzozo kamili utazuka.
Wanamgambo wa Hezbollah wa Lebanon waifyatulia Israel maroketi na droni
"Ikiwa Israel itaendelea kuwalenga raia, itatusukuma kurusha roketi na kulenga makazi mapya ambayo hayakulengwa hapo awali."
Kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP, tangu Oktoba mwaka jana, ghasia za mpakani zimeua watu 511 nchini Lebanon, wengi wao wakiwa wapiganaji pamoja na takriban raia 104. Kwa upande wa Israel, wanajeshi 17 na raia 13 wameuawa, kwa mujibu wa mamlaka.