1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hertha Berlin

Na Ramadhan Ali30 Mei 2007

Hertha Berlin ni timu ya Bundesliga ya daraja ya kwanza.Iliwahi kutawazwa mabingwa wa Ujerumani mara 2-mwaka 1930 na 1931.

https://p.dw.com/p/CHc7

Katika mtaa wa Stralsunder Strasse,Julai 25, 1892 vijana 4 wasiopindukia umri wa miaka 17 walikutana hapo kuunda klabu ya dimba –maarufu leo kwa jina la Hertha Berlin.Haukupita muda timu hii ilianza kutamba mjini Berlin na ikanyakua ubingwa wa Ujerumani hapo 1930 na tena 1931 kabla ya vita vya pili vya dunia.

“Timu zaingia uwanjani.Yatangulia Hertha BSC ikivalia kaptura nyeusi.Bingwa wa Berlin na wa Ujerumani kwa mara ya 6 mfululizo inacheza finali ya kuania taji la Ujerumani.Wingi wa shoto wa Berlin atupiwa mpira na bila ya kuchelewa afyatua mkwaju mkali na kuipatia Hertha BSC bao la ushindi.Kwa mara ya pili Hertha BSC imetoroka na ubingwa wa Ujerumani.”

Nahodha wao alikuwa wakati ule Hanne Sobeck, staid wao wa kwanza Hertha na aliesalia hivyo hadi kufariki kwake 1989.Kuna uwanja unaoitwa huko Berlin kwa jina lake-uwanja wa kale wa Hertha “Plumpe”.

Sobek:

“Nikiwa chipukizi kila mara nikikuka uwa wa senyenge kuingia uwanjani kwavile si kumudu fedha za kiingilio.Halafu ndoto yangu ya utotoni-dimba ikatimilia kwani baadae nikaanza kucheza mwenyewe uwanjani.”

Ubingwa wa Hertha Berlin wa miaka ya 1930 na 1931 ukabaki kwahivyo mataji 2 pekee iliotwaa timu hii hadi leo.Hatahivyo, Hertha ilisalia kuwa timu bora kabisa jijini humo.

1965 kwa mara ya kwanza pale uongozi wa Hertha Berlin ulipoanza kuwalipa wachezaji vitita vikubwa vya fedha,mambo yalianza kuwaendea kombo:Matokeo yake Hertha ililazimishwa kuteremshwa daraja ya pili.Kwani,Hertha ilijikuta katika kashfa ya dimba ya Bundesliga.Beki wao mshahara Bernd Pazke alitongozwa kwa fedha tena na klabu mbali mbali na akawa hajui afanye nini.

“mmoja kanitongoza kwa kitita cha DM alfu 1.Lakini, tayari kuna aliekwishajitolea kunipa kitita sawa na hicho. Zaidi yakafuata.Kwangu simu haikusita siku nzima kwahivyo sikamati simu.” Patzke alikumbusha.

Hivyo ndivyo anavyokumbusha beki mshahara Patzke mambo yalivyokuwa 1965.Kashfa hii haikuisadia Berlin kutamba katika Bundesliga na hata kwa mashabiki wake jijini berlin.Na hadi leo kuna mapenzi ya chuki kati ya mashabiki wa Hertha na klabu yao.Endapo Hertha ikishindwa mechi 2 mfululizo,mashabiki hulalamika kupita kiasi na endapo ikishinda mechi 3 mfululizo,basi mashabiki hao hao huanza kuandaa sherehe ya ubingwa.Hivyo ndivyo ilivyokua na desturi hii itaselelea.

Hertha ilikombolewa tena hapo 1989.Kwani,siku 2 baada ya kuporomoka kwa ukuta wa Berlin,Berlin ilicheza na Wattenscheid na ikafungua milango ya uwanja wake kwa maalfu ya mashabiki wa Berlin mashariki.

Hapo Hertha Berlin ikawafurahisha mashabiki waliotokwa na machozi kwa furaha.Miaka ya 1980 na nusu ya 1990,hertha Berlin ilipitisha katika daraja ya pili ya Bundesliga.Mara 2 lakini ilifaulu kucheza katika daraja ya kwanza na kurudi ya pili.

Kwa muda mrefu sasa Hertha Berlin inaongozwa na meneja Dieter Hoeness-ndugu wa meneja wa bayern Munich Uli Hoeness.Kitambo sasa amefaulu kuibakisha Berlin katika daraja ya kwanza ya Bundesliga.Ameshindwa lakini kuifanya timu hii ya jiji kuu kutamba na kuwa safu moja na klabu kama Bayern Munich,Hamburg au B.Dortmund.

Hertha Berlin ina maskani yake sio tena katika mtaa Stralsunder str. Ilikoasisiwa Julai 25,1892 bali katika Uwanja wa kisasa kabisa wa olimpik Stadium-kituo cha finali ya Kombe la dunia la FIFA mwaka jana.Hertha Berlin imetoka mbali ,lakini ina masafa pia marefu ya kuparamia kileleni mwa Bundesliga na kuwa mabingwa tena kama 1930 na 1931.