SiasaUkraine
Helikopta ya polisi ya Ukraine yaanguka na kuuwa watu 16
18 Januari 2023Matangazo
Helikopta ya jeshi la polisi la Ukraine imeanguka karibu ya shule ya chekechea na jengo la makaazi ya watu katika mji wa Brovary ulio nje kidogo ya mji mkuu, Kiev.
Gavana wa Kiev Oleksiy Kuleba amesema kuwa wakati wa mkasa huo watoto na walimu walikuwa madarasani, na duru za hivi karibuni zimeeleza kuwa watu wasiopungua 16 wameuawa, akiwemo waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine Denys Monastyrsky pamoja na watoto sita.
Maafisa wengine kadhaa wa wizara ya mambo ya ndani waliokuwa pamoja na waziri katika ndege hiyo pia wameuawa. Watu wengine 22 wamejeruhiwa, watoto 10 wakiwa miongoni mwao.