1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi na waasi wakabiliana nchini Mali

2 Oktoba 2023

Waasi wa Tuareg kaskazini mwa Mali wanadai kuteka kambi nyingine ya jeshi la Malia ikitawajwa kuwa ni ya nne tangu Agosti.

https://p.dw.com/p/4X1oZ
Mali Symbolbild Tuareg Rebellen
Picha: Souleymane Ag Anara/AFP

Kuongezeka kwa ghasia kunaendana na hatua inayoendelea ya kuondolewa kwa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kufanikisa amani nchini humo.

Kwa upande wake jeshi la Mali limesema jana Jumapili limekiri  kuhusika katika vita na waasi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa nchi hiyo.

Ripoti ya jeshi katika mitandao ya kijamii ilisema kumekuwa na 'mapigano makali' dhidi ya 'magaidi' katika eneo la Bamba ambalo waasi wanaotaka kujitenga wanadai kulidhibiti.

Kambi ya kijeshi ya Bamba huko Gao ni ya nne kuchukuliwa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyotekelezwa tangu Agosti na waasi wa kundi la harakati za Azawad.

Mashambulizi hayo yalifuatia kuondoka kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao ulisaidia kudumisha hali ya utulivu kwa miaka mingi.