Kocha wa Urusi Capello katika hali ngumu
15 Juni 2015Shirikisho la kandanda la Urusi linatafakari hatma ya Capello mwenye umri wa miaka 68 baada ya kichapo cha bao moja kwa sifuri dhidi ya viongozi wa Kundi G Austria na kuwaacha katika nafasi ya tatu pointi nne nyuma ya nambari mbili Sweden.
Uholanzi iliishinda Latvia magoli mawili kwa moja wakati England ikiifunga Slovania mabao matatu kwa mawili. Katika matokeo mengine ya mechi za jana Sweden iliifunga Montenegro mabao 3-1. Uhispania ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Belarus nayo Uswisi ikaibwaga Lithuania kwa mabao 2-1. Ukraine iliangusha Luxembourg mabao 3-0.
Katika michezo ya Jumamosi Ujerumani iliiangamiza Gilbratar kwa kuitandika magoli 7-0 nayo Poland ikailaza Georgia mabao 4-0. Scotland na Jamhuri ya Ireland zitoka sare ya bao 1-1.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Iddi Ssessanga