1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Soka. AC Milan yapewa ushindi na UEFA.

14 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNG

Shirika la kandanda barani Ulaya UEFA, limeithibitisha timu ya AC Milan ya Italy kuwa mshindi wa pambano la champions League la robo fainali dhidi ya Inter Milan pia ya Italia. Mchezo huo ulikatishwa siku ya Jumanne baada ya dakika 73 kufuatia ghasia zilizofanywa na mashabiki.

Katika wakati huo AC Milan ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0. Mashabiki wa Inter walirusha uwanjani fashfash , na kusababisha mlinda mlango wa AC Milan kuumia. Inter inatarajiwa kupigwa marufuku kuutumia uwanja huo wa nyumbani kwa mechi kadha msimu ujao.

Katika mchezo wa Jumanne wa marudiano kati ya Liverpool na Juventus Turin nayo ya Itali, sare ya bila kufungana ilitosha kuipitisha Liverpool katika nusu fainali, baada ya timu hiyo kushinda kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza. Liverpool itakutana na Chalsea katika nusu fainali na AC Milan itapambana na PSV Eindhoven baada ya timu hiyo kuishinda Olympique Lyon ya Ufaransa kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kwenda sare katika michezo yote miwili.