Hatimaye kampuni ya Canada yashinda:
10 Septemba 2009Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magari ya Marekani Generel Motors imeamua kuliuza tawi lake la Ujerumani,Opel kwa kampuni ya Canada ,Magna International.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amethibitisha uamuzi huo aliokuwa anaupendelea wakati wote.
Akizungumza na waandishi habari mjini Berlin Kansela Merkel alithibitisha uamuzi wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya General Motors. Kiongozi huyo wa Ujerumani amefurahishwa na uamuzi huo.
Uamuzi wa bodi hiyo unamaliza hali ya wasiwasi iliyokuwa inawakabili wafanyakazi 25,000 wa tawi la Opel la Ujerumani.
Serikali ya Ujerumani wakati wote imekuwa inaiunga mkono kampuni ya Canada Magna International na imesema itatenga kiasi cha Euro bilioni 4 .5 kama dhamana ya kuisaidia kampuni hiyo katika juhudi za kuleta muundo mpya kwenye tawi.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema anaamini kuwa pendekezo hilo litakubalika kwa General Motors.
Kampuni ya GM imesema itadumisha asilimia 35 ya hisa na itauza asilimia 55 kwa kampuni ya hiyo ya Magna. Wafanyakazi watamikili asilimia 10 katika kile General Motors ilichoita Opel mpya.
Mwandishi:Meyer-Feist,Andreas/Wien (ARD)
Mtafsiri:A.Mtullya
MhaririM.Abdul-Rahman