1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya Pistorius kujulikana Septemba 11

12 Agosti 2014

Wakili wa Oscar Pistorius mwanariadha anayekimbia kwa miguu ya bandia amesema jana Ijumaa kuwa , "ukweli unaonekana wazi," hauwezi kuthibitisha kuwa mkimbiaji huyo alikuwa na nia ya kumuua rafiki yake wa kike

https://p.dw.com/p/1CszZ
Oscar Pistorius 8.7.14
Picha: Reuters

Hiyo ni wakati wakili huyo akichukua hatua ya mwisho kumuokoa mwanariadha huyo dhidi ya kifungo cha maisha.

Katika maelezo yake wakati wa akifunga hoja yake , wakili huyo Barry Roux amejaribu kuvunja madai ya upande wa mashtaka kuwa mteja wake alimuua kwa makusudi Reeva Steenkamp aliyekuwa na umri wa miaka 29 baada ya kutokea kutokuelewana alfajiri ya siku ya wapendanao mwaka 2013.

Ushahidi wa mwisho umeelezea upande usiofahamika kabisa wa Oscar, mwenye umri wa miaka 27, kwamba alimpiga Reeva risasi nne akiwa kwenye bafu akiwa hasa na dhamira ya kumuua. Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, Oscar ni "mdanganyifu" mwenye kipaji cha kudanganya. Jaji Thokozile Masipa atatoa hukumu ya kesi hiyo tarehe 11 mwezi Septemba.

Mwandishi: Sekione Kitojo/AFP
Mhariri: Josephat Charo