Hassan Rouhani ashinda uchaguzi wa rais Iran
21 Mei 2017Wizara ya mambo ya ndani ya ndani ya Iran imemtangaza Rais Hassan Rouhani kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais kwa kumshinda mpizani wake wa msimamo mkali Ebrahim Rais kwa kujitzolea zaidi ya kura milioni 22 dhidi ya zadi ya miloni 15.
Rouhani mwenye umri wa miaka 68 mwanamageuzi aliyeiongoza nchi yake kufikia makubaliano ya kihistoria na nchi sita zenye nguvu zaidi duniani kuhusu mpango wake wa kinyuklia ameshinda uchaguzi huo uliofaniyka hapo jana kwa asilimia 57 ya kura.
Amemshinda mpinzani wake mkuu Ebrahim Raisi ambaye alikuwa anaungwa mkono na baraza lenye ushawishi mkubwa la masheikh wa kiislamu wasiochaguliwa kupitia chaguzi. Uchaguzi huo umetajwa kama kura ya maoni ya kupima utendaji wa Rouhani kuhusu juhudi zake za kuifungulia fursa nchi yake kwa mataifa ya magharibi. Kituo cha televisheni cha Iran kimempongeza Rouhani kwa ushindi huo unaombakisha madarakani.