1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harusi ya Mwanamfalme William na Kate wa Uingereza

29 Aprili 2011

Ni Rasmi, Mwanamfalme William na mpenzi wake, Katherine ni mke na mume. Wawili hao walizifunga pingu zao za maisha mapema hii leo katika kanisa kuu la Westminster Abbey lililo katikati ya mji wa London.

https://p.dw.com/p/116aK
Mwanamfalme William akimbusu mkewe Kate Middleton katika kasri la BuckinghamPicha: dapd

Mamilioni ya watu walilishuhudia tukio hilo la kihistoria kwenye eneo lililo karibu na kanisa, kadhalika kwenye televisheni. Muda mfupi baada ya kuozwa, Mwana mfalme William alimbusu mkewe Kate Middleton waliposimama kwenye roshani ya Kasri la Buckingham wakati ndege za kijeshi zilipopuruka angani kwa heshima ya Mwanamfalme William. Ili kupata picha halisi ya mambo yalivyokwenda Thelma Mwadzaya alizungumza na Suleiman Salim, mkaazi wa jiji la London wa muda mrefu na mwandishi wa habari...