1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris na Trump washikana mikopo kumbukumbu ya 9/11

12 Septemba 2024

Wagombeahi hao wawili wa urais walipeana mikono ikiwa ni mara ya pili kuonana hadharani baada ya mdahalo.Ilikuwa ni onyesho thabiti la umoja.

https://p.dw.com/p/4kWwT
Marekani New York 2024 | Sherehe ya Kumbukumbu ya 9/11 | Kupeana mkono Kamala Harris na Donald Trump
Trump na Harris wakisalimiana kwa kupeana mikono.Picha: Mike Segar/REUTERS

Wagombea urais wa Marekani Kamala Harris na Donald Trump wamekutana tena katika Kumbukumbu ya Mashambulizi ya Septemba 11, muda mfupi baada ya wawili hao kushiriki mdahalo mkali jioni iliyotangulia.

Harris na Trump walisimama pamoja mjini New Yok wakati wa kumbukumbu hiyo, na kisha kushikana mikono, ikiwa ni mara ya pili kuonana hadharani.

Rais wa Marekani Joe Biden alihudhuria kumbukumbu hiyo, ambayo ilihudhuriwa pia na mgombea mwenza wa Trump, J.D Vance.

Kabla ya kuhudhuria kumbukumbu hiyo ya Septemba 11, Trump alionesha kukasirishwa na utendaji wake kwenye mdahalo wa televisheni ambapo wadadisi walisema alishindwa na Kamala Harris.