1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Upinzani huenda ukaafikiana na Rais Mugabe

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAX

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai anaeleza kuwa kuna uwezekano kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika kati ya chama chake na Rais Mugabe huenda yakafua dafu.Mazungumzo hayo yananuia kuondoa mkwamo wa kisiasa unaokumba nchi hiyo.

Matatizo ya kisiasa nchini humo yaliongezeka mwezi jana baada ya mawakala wa usalama wa serikali kumshambulia Morgan Tsvangirai na wafuasi wake mjini Harare wqalikokuwa wakifanya mkutano.

Bwana Tsvangirai alikiri kupokea barua kutoka kwa Rais Mbeki wa Afrika Kusini aliye mpatanishi kufuatia kikao maalum cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC mjini Darsesalam nchini Tanzania.Kikao hicho kilijadilia tatizo la Zimbawe mwezi jana.

Wafuasi kadhaa wa upinzani wa chama cha MDC wamekamatwa na kuzuiliwa na kudaiwa kuteswa katika kipindi cha majuma yaliyopita bnaada ya kulaumiwa kushambulia maduka na vituo vya polisi.Chama cha MDC kinampa Rais Mugabe upinzani mkali sana tangu aingie madarakani mwaka 80