HARARE:Rais wa Zimbabwe atakiwa kujiuzulu
10 Agosti 2005Waziri wa zamani wa habari nchini Zimbabwe Jonathan Moyo leo amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu akisema Mugabe amekosa kuitambua hali halisi ya nchi kufuatia kukataa kwa rais huyo kufanya mazungumzo na upande wa upinzani.
Moyo amesema rais mugabe na chama chake cha Zanu Pf kinastahili kujiondoa madarakani na kuwaachia nafasi ya kujiamulia kwa njia ya amani,kidemokrasia na kikatiba wananchi wa zimbabwe na kuuyatatua matatizo yao.
Rais Mugabe mapema wiki hii alikataa kufanya mazungumzo na chama cha upinzani cha Movemement for Demokratic Change juu ya mzozo wa taifa na kukitaja kuwa chama cha vibaraka wa serikali ya Uingereza.
Badala yake rais Mugabe aliyeitawala Zimbawe kwa miaka 25 alisema bora kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair kuliko chama hicho cha upinzani.
Zimbabwe inakabiliwa na matatizo kadha ikiwa ni pamoja na upungufu wa chakula na mafuta,na kuwa na idadi kubwa ya watu wasioajira.