1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Rais Obasanjo awasili Zimbabwe

17 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CG0K
Rais Olesegun Obasanjo wa Nigeria amewasili katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare mapema leo hii kwa mazungumzo ya kutwa moja na Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo kabla ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola mwezi ujao ambapo hadi hivi sasa Mugabe hakualikwa. Mkutano wa kila mwaka wa Viongozi wa nchi na serikali wa Jumuiya ya Madola mwaka huu unatazamiwa kufanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja katika kipindi cha wiki tatu zijazo. Zimbabwe imesimamishwa uwanachama wa Jumuiya hiyo ya Madola kwa miezi 20 sasa kufuatia uchaguzi wa Rais wa mwezi wa Machi mwaka 2002 ambao umemrudisha Mugabe madarakani uchaguzi ambao upinzani na sehemu kubwa ya jamii ya kimataifa unasema umekuwa na ukiukaji mkubwa wa taratibu. Obasanjo kama mwenyeji wa mkutano huo wa Jumuiya ya Madola anashikilia funguo za mialiko nchini Nigeria.