1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:MDC yakabiliwa na tuhuma za kupokea fedha kutoka nje.

26 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEOO

Serikali ya Zimbabwe imo mbioni kuchunguza tuhuma kuwa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Movement for Democratic Change-MDC kilipokea kinyume cha sheria dola milioni 2.5 kutoka mataifa matatu ya kigeni.

Mbunge mmoja wa chama hicho cha MDC Job Sikhala,amedai kuwa chama chake hivi karibuni kimepokea fedha hizo kinyume cha sheria kutoka Ghana,Nigeria na Taiwan.

Sheria za Zimbabwe zinakataza chama chochote cha siasa nchini humo kupokea fedha kutoka nje.

Hata hivyo chama cha MDC kimekanusha madai hayo na kusema kamwe hakijawahi kupokea hata senti moja kutoka nje ya nchi hiyo na kwa mujibu wa msemaji wa rais wa chama William Bango,Mbunge huyo Sikhala anahitaji kupimwa akili.

Hata hivyo mbunge Sikhala ameeleza zaidi kuwa kupatikana kwa fedha hizo,ndio chanzo cha mgawanyiko uliopo ndani ya chama hicho,ambapo zaidi ya nusu ya wanachama wameupinga ushauri wa kiongozi wao Morgan Tsvangirai wa kuususia uchaguzi wa Bunge la Senate uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi ujao.