HARARE:Banana Rais wa zamani Zimbabwe afariki
11 Novemba 2003Matangazo
Rais wa kwanza mzalendo wa Zimbabwe Canaan Banana amefarika hapo jana rafiki yake wa karibu wa zamani Rais Robert Mugabe ametangaza katika taarifa iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa
Mugabe amemwelezea Banana ambaye alikuwa madarakani kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1987 kuwa ni zawadi adimu kwa taifa lao. Banana mwenye umri wa miaka 67 amekuwa akiuguwa kwa muda mrefu.Mugabe ambaye alikuwa waziri mkuu wakati Banana akiwa Rais na baadae kuchukuwa madaraka kutoka kwake hapo mwaka 1987 amesema mtangulizi wake huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali za Afrika Kusini.
Banana aliingia katika fedheha zaidi ya muongo mmoja baada ya kuondoka madarakani ambapo alitiwa mbaroni nchini Zimbabwe hapo mwaka 1996 kwa madai ya kumdhalilisha kingono mlinzi wake wa zamani Jefta Dube.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani na Mahkama Kuu hapo mwaka 1999 lakini alitumikia kifungo cha miaka miwili tu na aliachiliwa hapo mwaka 2001 ambapo baada ya hapo alikuwa hasikiki sana.