HARARE:Amnesty Inernational lautaka Umoja wa Mataifa kuwaokoa wananchi wa Zimbabwe
24 Juni 2005Matangazo
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International pamoja na mashirika mengine kiasi ya 200 ya Afrika na kimataifa yameutaka Umoja wa Mataifa na viongozi wa Afrika kuzuia uvunjwaji wa nyumba kwa nguvu na serikali, nchini Zimbabwe.
Hatua hiyo ya serikali ya Zimbabwe iliyochukua wiki sita tayari imesababisha watoto wawili kufariki kutokana na maporomoko wakati wa kuvunjwa nyumba hizo .
Maelfu ya watu nchini Zimbabwe wameachwa bila makaazi kutokana na hatua hiyo.
Umoja wa Mataifa tayari wamepeleka mjumbe maalum kuchunguza hali ya kibinadam.Wakosoaji wamesema hatua hiyo imezidisha mzozo wa uchumi wa Zimbabwe,huku pesa za kigeni zikipungua na kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na asilimia kubwa ya ukosefu wa ajira.