HARARE Zimbabwe yawakataza viongozi wa upinzani wa Afrika Kusini kuingia nchini humo..
18 Februari 2005Matangazo
Zimbabwe imewakataza wajumbe wa chama kikuu cha upinzani cha Afrika Kusini wasiingie nchini humo, ikisema hawana kibali cha kuingia taifa hilo. Chama cha DA kikiongozwa na wakili Tony Leon, kilitaka kuchunguza ikiwa uchaguzi unaotarajiwa tarehe 31 mwezi Machi nchini Zimbabwe unaweza kufanyika kwa njia huru na ya haki.