1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Zimbabwe yakaribia kufanya uchaguzi lakini kuana malalamiko.

16 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFWR

Umoja wa nchi za Afrika utapeleka wawakilishi kushuhudia uchaguzi wa Zimbabwe unaotarajiwa kufanyika mwisho wa mwezi machi.

Ujumbe wa watu kumi utasafiri hadi Harare tarehe 25 mwezi machi kufuatia mualiko kutoka kwa serikali ya Zimbabwe kwa mataifa 53 wanachama wa umoja wa nchi za Afrika.

Uchaguzi huu ni mtihani mkubwa kwa rais Robert Mugabe ambae ameahidi kuwepo uchaguzi huru na wahaki.

Rais Mugabe ameyaalika mataifa 32 na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali 13 kuja kusimamia uchaguzi huo nchini Zimbabwe.

Tayari mashirika ya kimataifa yameeleza wasiwasi wao kwamba na kwamba hadi sasa hakuna dalili zanazoonyesha kuwepo na uchaguzi huru na wa haki nchini Zimbabwe.