1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Zimbabwe yailalamikia ripoti ya umoja wa mataifa.

23 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErZ

Serikali ya Zimbabwe imeilalamikia ripoti ya umoja wa mataifa inayoilaumu serikali hiyo kwa kuvunja vibanda vilivyojengwa na wananchi katika miji.

Zimbabwe imesema ripoti hiyo ya umoja wa mataifa imeelemea upande moja na si sahihi, na uvunjaji huo ulikuwa muhimu ili kudhibiti hali ya ukosefu wa amani.

Ripoti hiyo inasema kuwa uvunjaji huo unakwenda kinyume na sheria za kimataifa , na umesababisha maafa ya kibinadamu.

Inasema pia kuwa zoezi hilo limesababisha watu 700,000 kukosa makaazi pamoja na ajira. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan ameitaka serikali hiyo kuacha kuwaondoa wananchi hao mara moja.