1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Wanawake wa Zimbabwe wateseka

26 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfB

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema wanawake wa Zimbabwe wanateseka huku hali ya uchumi ikiendelea kuwa mbaya nchini humo.

Shirika hilo limetoa ripoti yake inayosema mamia ya wanawake wamekamatwa bila makosa, kuhujumiwa kimwili na kunyimwa chakula kwa kuikosoa serikali ya Zimbabwe.

Ripoti hiyo pia imebaini kuwa watetezi wengi wa haki za binadamu nchini Zimbabwe ni wanawake.

Shirika la Amnesty International limewataka wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, zitumie mkutano ujao wa kilele wa Umoja wa Afrika kuishinikiza serikali ya rais Robert Mugabe ikomeshe mateso dhidi ya watetezi wanawake.