1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Viongozi wa upinzani wakamatwa Zimbabwe

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK1

Nchini Zimbabwe,polisi wamewakamata viongozi kadhaa wa upinzani na wamempiga risasi na kumuuwa mtu mmoja,wakati wa kuuvunja mkutano wa kutaka kusali hadharani.Kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC,bwana Morgan Tsvangirai na maafisa wengine wa upinzani,walikamatwa walipokuwa njiani kwenda kuhudhuria mkutano uliopangwa kufanywa kwenye uwanja wa michezo mjini Harare.Mashahidi wamesema,polisi wenye silaha nzito walipambana na wafuasi wa upinzani waliokuwa wakirusha mawe. Wameongezea kuwa hata wanafunzi wanaopinga utawala wa Mugabe wamekamatwa.Rais Mugabe wa chama cha ZANU-PF anatawala tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1980. Upande wa upinzani unataka mabadiliko ya kisiasa nchini Zimbabwe.