1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Upinzani waapa kumn’gowa Mugabe

17 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIL

Upinzani nchini Zimbabwe umeapa kuendeleza kampeni yao hadi mwisho kumn’gowa madarakani Rais Robert Mugabe wakati kiongozi wao akitoka hospitali baada ya kupata mkon’goto wa polisi.

Kiongozi wa chama cha upinzanui cha MDC Morgan Tsvangirai akizungumza na shirika la habari la Uingereza Reuters akiwa nyumbani kwake baada ya kutoka hospitali amesema ataendelea kupambana hadi mwisho kukomesha utawala wa muda mrefu wa Mugabe na kwamba uhuru sio kitu rahisi.

Tsvangirai na wafuasi kadhaa wa upinzani walikamatwa wakiwa njiani kuelekea kwenye mkutano wa hadhara dhidi ya Mugabe hapo Jumapili.

Rais Mugabe amesema kwamba wapinzani watakabiliwa na mkon’goto zaidi iwapo watafanya maandamano zaidi na pia kuwaonya wanadiplomasia wa nchi za magharibi wanaomuunga mkono Tsvangirai wawe na nidhamu nzuri venginevyo watatimuliwa nchini humo.