1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE. Upinzani nchini Zimbabwe waongoza katika matokeo ya mwanzo ya uchaguzi.

1 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFRI

Upinzani nchini Zimbabwe umeshinda katika miji muhimu, dhidi ya chama cha ZANUPF, kinachoongozwana rais Robert Mugabe. Chama cha Movement fof Democratic Change, kikiongozwa na Morgan Tsvangirai, kilijipatia viti 17 kati a 19, hivyo kushinda katika miji a Harare na Bulawayo, kama ilivyofanyika mwaka wa 2000. Chama cha ZANUPF, kimejishindia viti viwili katika eneo la kazkazini la Mashonaland na eneo la mashariki la Marondera, ambako kina wa wafuasi wengi. Ijapo rais Robert Mugabe anasema uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa huru na wa haki, na kwamba hakukuwa na visa vingi vya machafuko ikilinganishwa na uchaguzi uliopita, umoja wa Ulaya na Marekani, ziliutaja uchaguzi huo kuwa wa bandia. Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe imesema kadri asilimia kumi ya watu walizuiliwa kupiga kura zao katika vituo vya kupigia kura, pasipo sababu yoyote maalumu kutolewa. Lakini mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema idadi ya raia waliozuiliwa kupiga kura ni kubwa zaidi, na huenda ni asilimia 25 ya wapiga kura wote.