HARARE: Uchaguzi wa zimbabwe sio halali Marekani yasema
6 Aprili 2005Marekani bado inashikilia uchaguzi wa wabunge nchini Zimbabwe haukufanyika kwa njia ya haki wala uhuru licha ya kukubalika na mataifa jirani.
Msemaji wa idara ya mambo ya ndani wa Marekani Richard Boucher amepinga uamuzi uliotolewa na tume ya waangalizi nchini humo kutoka jumuiya ya maendeleo ya Afrika SDDC kwamba matokeo yametokana na uamuzi wa wananchi wa Zimbabwe.
Uchaguzi huo ambapo chama cha rais Mugabe kilishinda kwa ukubwa ulifanyika bila ghasia lakini Boucher anasema Kampeini zilipendelea sana upande wa serikali.
Matamshi ya Boucher yamefuatia maandamano ya vijana katika mji wa Harare ya kuwataka wananchi kuyapinga matokeo ya uchaguzi.
Hata hivyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka pande zote mbili kuzungumza na kutatua mzozo huo.Wakati huo huo wanahabari wawili wa Uingereza waliokamatwa nchini Zimbabwe kwa madai ya kuingia nchini humo bila ruhusa wamechiwa huru baada ya kukosekana na hatia.