1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : SADC yaidhinisha uchaguzi wa Zimbabwe

3 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQd

Nchi jirani na Zimbabwe leo hii zimeidhinisha matokeo ya uchaguzi wa bunge ambapo chama tawala cha Rais Robert Mugabe kimejizolea ushindi mkubwa na kutupilia mbali madai ya hujuma na shutuma za Marekani,Uingereza na serikali za mataifa ya magharibi.

Timu ya waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi 11 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC imesema kwamba uchaguzi huo umeonyesha matakwa ya wananchi licha ya kuwepo kwa upendeleo na vyombo vya habari na matatizo mengine ya upigaji kura.

Uamuzi wa timu hiyo inayoongozwa na Afrika Kusini unaiweka katika mkondo wa kuhitilafiana na Marekani,Uingereza Canada na Umoja wa Ulaya ambazo zimetangaza kwamba uchaguzi huo haukuwa huru wala wa haki.

Chama tawala cha ZANU-PF kimejishindia wingi wa theluthi mbili ya viti katika uchaguzi huo wa Alhamisi ambapo chama cha upinzani cha MDC kimeushutumu kuwa wa udanganyifu mkubwa.