1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare. Rais Mugabe atetea uamuzi wa kuwavunjia watu waliojenga ovyo katika mji wa Harare.

10 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF58

Rais wa Zimbabwe Bwana Robert Mugabe jana aliutetea uamuzi wa hivi karibuni wa kuvunja vibanda na kuwafukuza wafanyabiashara wadogo wadogo barabarani katika mji mkuu Harare kuwa ni sehemu ya juhudi za serikali yake za kupambana na rushwa na kuinua kiwango cha nafasi ya wazalendo katika uchumi wa nchi hiyo.

Bwana Mugabe alikuwa akizungumza katika ufunguzi rasmi wa bunge jipya ambapo chama kikuu cha upinzani kimeususia kama sehemu ya mgomo wa siku mbili katika kupinga dhidi ya msako huo ambao wakosoaji wanasema umewakosesha mamia kwa maelfu ya watu mahali pa kuishi na uwezo wa kujipatia fedha.

Maelfu ya watu wamekamatwa na wengine kadha wameharibiwa sehemu zao za kibiashara pamoja na bidhaa zao kukamatwa katika kile serikali ilichosema kampeni ya kuondoa uhalifu ikiwa ni pamoja na biashara haramu ya fedha za kigeni na bidhaa muhimu kama sukari ambayo imekuwa adimu kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.