1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harare: Polisi wa Zimbabwe wawakamata wakuu wa vyama vya ...

19 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzz
wafanyakazi Polisi wazuia fujo jana waliwakamata viongozi wa shirika kuu la vyama vya wafanyakazi na darzeni kadha za wanaharakati wanaogombea haki za kiraia kile pembe ya Zimbabwe na kutawanya maandamano dhidi ya kuimarika mzozo wa kiuchumi, walisema maafisa wa vyama vya wanfanyakazi. Shirika la vyama vya wafanyakazi nchini Zimbabwe ZCTU lilisema polisi waliwakamata zaidi ya watu 360 katika mji mkuu Harare na miji kadha mingine nchini humo. Vyama vya wafanyakazi viliongoza maadanamano dhidi ya kupanda kwa kadiri kubwa bei ya mafuta, huku serikali ya Rais Robert Mugabe ikikabiliana na shida za uhaba wa fedha za kigeni, ukosefu wa ajira na kimoja kati ya viwango vikubwa kabisa duniani kuhusu mfumko wa bei za vitu ambao katika mwezi wa Oktoba uligonga asilimia 525. Mamia ya polisi, wangi wakiwa na bunduki za automatik, walipiga doria mjini Harare kabla ya maandamano, ambayo yaliitishwa na shirika ZCTU kabla ya kutangazwa bajeti ya serikali hii leo.