1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Mugabe apuuza lawama za wakosoaji wa kimataifa

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIf

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewashambulia wakosoaji wake na amepuuza lawama zilizotolewa na jumuiya ya kimataifa kuhusika na kukamatwa na kupigwa kwa kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai.Mugabe mwenye umri wa miaka 83 amekituhumu chama cha Tsvangirai cha MDC kuhusika na vitendo vya ghasia vilivyosababisha kukamatwa kwake siku ya Jumapili.Tsvangirai yupo hospitali kwa matibabu ya majeraha ya kichwani aliyopata wakati alipokuwa mikononi mwa polisi.Nchi za magharibi zinafikiria kuweka vikwazo zaidi dhidi ya Zimbabwe kwa sababu ya madai kwamba hatua kali zilichukuliwa dhidi ya wanaharakati wa upinzani.