1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE : Mugabe akaripia wanaowania kumrithi

15 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjB

Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe amekaripia wanachama wa chama chake tawala cha ZANU –PF kwa kuendeleza mapambano miongoni mwao ya kuwania kurithi nafasi yake kwa kusema kwamba suala hilo la kurithi nafasi yake linaweza kukiangamiza chama hicho.

Mugabe ambaye hivi karibuni alidokeza shauku ya kuongeza muda wa utawala wake kupíndukia mwaka 2008 ambapo uchaguzi wa Urais ulikuwa umepangwa kufanyika amesema wakati wa mkutano wa kamati kuu ya chama hico mjini Harare hapo jana kwamba hakuna nafasi ilio wazi kwenye wadhifa huo wa juu kabisa.

Gazeti la serikali la Herald limemkariri Mugabe akimwambia Makamo wake Rais Jospeh Msika kwamba suala hilo la kugombania kurithi nafasi yake linaleta matatizo na amewataka wasite kufanya hivyo.

Mugabe leo anatazmiwa kuhutubia wa kila mwaka wa chama cha ZANU- PF katika mji wa Goromonzi karibu na Harare ambapo anatarajiwa kuelezea mipango yake ya kujiuzulu.