HARARE: Maripota 2 wa Kingereza waachiliwa huru Zimbabwe
16 Aprili 2005Matangazo
Waandishi habari wawili wa Kingereza waliofikishwa mahakamani nchini Zimbabwe kwa mashtaka ya kuripoti uchaguzi wa mwezi uliopita bila ya ruhusa,wameachiliwa huru.Hakimu,Never Diza amesema,waendesha mashtaka wameshindwa kuthibitisha kuwa Toby Harnden na Julian Simmonds wamefanya kazi nchini,kinyume na sheria.Watu hao wawili waliokamatwa karibu na mji wa Harare siku ya uchaguzi,waliachiliwa kwa dhamana baada ya kuwekwa jela kwa wiki mbili.Waingereza hao wamesema walikuwa wakiizuru Zimbabwe kama watalii.Wapelelezi wa serikali walizuia kompyuta za mkono na kamera,lakini hawakuweza kufasiri hati-mkato.Kamera nayo haikuwa na picha.